![](http://www.itv.co.tz/media/image/mwalimu%282%29.jpg)
Chama
cha walimu tanzania (CWT)mkoani Kagera kimewaomba viongozi wa watakao
chaguliwa kusimamia serikali ijayo kuhakikisha inalipa deni sugu la
malimbikizo ya mishahara ya walimu ambapo mpaka sasa walimu wa mkoa wa
Kagera wanazidai halmashauri za wilaya na maspaa zaidi ya shilingi
bilioni tatu.
Hayo yamesemwa katika maadhimisho ya siku ya walimu duniani na
katibu wa chama walimu mkoani Kagera Posian Gelvas amesema walimu
wanapata shida katika kudai malimbikizo ya mishahara yao huku serikali
ikiwalipa wanasiasa mabilioni ya pesa ambazo zingeweza kusaidia kulipa
malimbikizo ya mishahara ya walimu ambayo wanaidai serikali miaka yote
na pia zingeweza kuboresha madarasa pamoja na kununua vitendea kazi
mashule jambo ambalo wamesema niaibu kubwa kwa serikali kuona baadhi ya
shule zinakosa hata chaki zakufundishia wanafunzi.
Mwenyekiti wa chama cha walimu mkoani kagera Dauda Bilikesi
akizungumza katika maadhimisho hayo yaliyofanyika kimkoa wilayani Kagara
amesema matatizo ya malimbikizo ya mishahara kwa walimu yanasababishwa
na baadhi ya waajili wazembe wanaokiuka sheria na kutozingatia kanuni
na sheria za utumishi wa umama ambapo amebainisha baadhi ya changamoto
ambazo zimekuwa zikigonga vinchwa vya walimu kila kukichwa kuwa ni
mishahara midogo isiyoendana na wakati wa sasa pamoja na walimu wastaafu
kutothaminiwa baada ya utumishi wao kwa muda mrefu.
Mkuu wa mkoa wa kagera john mongella ambae alikuwa mgeni rasmi
katika maadhimisho hayo amesema amelichukua suala hilo nakuwathibitishia
walimu kuwa kwaanzia sasa atalisimamia kidete nakwamba atahakikisha
halmashauri zote za wilaya na manispaa za mkoa wa kagera zinakaa na
walimu kwa pamoja ilikuweza kujadili namna ya kuwalipa walimu madai yao.
Maadhimisho haya walimu hufanywa na walimu kote duniani ambapo
zaidi ya nchi 166 zenye jumla ya vyama vya walimu takribani mianne
vikiwa na wanacha milioni therasin na tano ulimwenguni hufanya maadhisho
haya huku chama cha walimu Tanzania (CWT) kikitajwa kuwa nimiongoni
mwa wanachama hai wa shirikisho hilo.
Post a Comment