Mamlaka ya udhibiti wa chakula na dawa Tanzania TFDA kanda ya mashariki imearibu takribani tani 3 za bidhaa feki ikiwa pamoja na maziwa ya watoto zilizokamatwa zaidi ya Supar Maket 126 jijini Dar-es-Salaam.
Wakizungumzia juu ya kukamatwa kwa bidhaa hiyo wakaguzi wa TFDA wamesema jumla ya maduka 40 kati 126 yamekutwa hayana vibali vya biashara na kuuza maziwa ya watoto ambayo yapo chini ya kiwango ikiwa pamoja na kutokuwa na lebo huku wakisema mzigo huo ulioaribiwa ulikuwa na thamani ya takiribani zaidi ya milioni 34. 
 
Aidha wakaguzi hao wametoa wito kwa wafanya biashara wote nchi nzima kuwa makini na baadhi ya bidhaa zote zinazoingizwa nchini kinyume cha utaratibu unaokidhi viwango usika vya mamlaka ikiwa na kuwa pamoja na kuwa na vibari vyote usika kabila ya kufungua maduka yao.

 

Post a Comment