Tume ya taifa ya uchaguzi imesema haitaruhusu mawakala wa vyama vya NCCR-Mageuzi, CUF na NLD kuingia katika nyumba vya kuhesabia kura za wagombea urais kwa kuwa havina mgombea wa nafasi katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano ya viongozi wawakilishi wa wanawake, mkurugenzi wa tume ya uchaguzi Bwana Kailima Kombey, amesema tume ya taifa ya uchaguzi haitambui umoja wa katiba ya wananchi-UKAWA- bali inamtambua kisheria mgombea urais kwa tiketi ya chama cha demokrasi na maendeleo-Chadema- chama ambacho kinapaswa kuteua mawakala wa kuwasimamia wagombea. 
 
Kuhusu hofu ya uwazi katika upigaji na kuhesabu kura, mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi, jaji mstaafu Damian Lubuva amesema kura zote zitapigwa na kuhesabiwa katika vituo chini ya usimamizi wa mawakala wa vyama na waandishi wa habari wataruhusiwa kuingia, na kusisitiza vyama vya siasa vinavyoshawishi wapigakura wao kubaki katika vituo kulinda kura vinaajenga ya kusababisha usumbufu na uwoga kwa baadhi ya wananchi utakaosababisha kutojitokeza kupiga kura.
 
Mwakilishi wa mtandao wa asasi za kirai mkoani Tanga Bi.Adela Mtei ameilalamikia tume ya taifa ya uchaguzi kwa kukaa kimya huku baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa wakitoleana na matusi na kashfa badala kutangaza sera hali inayotoa hofu kwa wanawake kuweza kujitokeza Oktoba 25 kutimiza haki yao ya kisheria ya kuchagua viongozi wanaowataka.
 

Post a Comment