“ Msilinde kura kwa kubaki Vituoni “ – Tume ya Taifa ya Uchaguzi
Tume ya Taifa ya uchaguzi nchini Tanzania – NEC imevitaka vyama vya siasa kuacha kuwahamasisha wapiga kura kubaki karibu na vituo vya kupigia kura kwa kigezo cha kulinda kura jambo ambalo ni kinyume cha sheria, kanuni na maadili ya uchaguzi na sababu za kiusalama.

Tume imetoa wito huo katika mkutano na vyama vya siasa jana jijini Dar es salaam, uliolenga kuelezea maandalizi ya uchaguzi na namna tume inavyotumia utaratibu wa kutangaza matokeo ya Udiwani, Ubunge pamoja na Urais.

Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano huo, Mwenyekiti wa tume hiyo Jaji Mstaafu Damian Lubuva, ametahadharisha kuwa endapo vyama vya siasa vitaruhusu wapiga kura kubaki vituoni kwa lengo la kulinda kura, upo uwezekano wa kutokea fujo kwani kwa uzoefu sehemu yenye mikusanyiko ndio fujo zinapoanzia.



Post a Comment