Mbowe – ” Mkimaliza kupiga Kura Wanawake mrudi Nyumbani Kupika, Wanaume wabaki kulinda kura “.

Akizungumza jana na umati mkubwa uliofika kushuhudia kampeni za UKAWA katika viwanja vya Tanganyika Parkers, Kawe jijini Dar es Salaam, Mweneyekiti wa chama cha CHADEMA Freeman Aikael Mbowe amesema ifikapo oktoba 25 baada ya kupiga kura, basi ni vyema wakina Mama warudi nyumbani kwa ajili ya kupika na Wanaume wabaki vituoni ili kulinda kura.

 

Mbowe amesema oktoba 25 si siku ya kulala hivyo amewataka wafuasi wa vyama vianavyounda umoja wa katiba ya wananchi – UKAWA wajitokeze kwa wingi katika kupiga kura na kuhakikisha hawaibiwi kura zao.
“ Oktoba 25, wakina Mama mkishamaliza kupiga kura ni bora mkarudi nyumbani kwa ajili ya kupikia awatoto na wazee, lakini wakina Baba mkimaliza kupiga kura hakikisheni mnahesabu mita 100 toka kwenye kituo cha kupiga kura na kukaa hapo kwa ajili ya kulinda kura zenu ”, alisema Mbowe.
Katika mkutano huo vingozi mbali mbali wa UKAWA wakiongozwa na mgombea wao urais Mh. Edward Lowassa walipanda jukwaani na kunadi sera zao ambapo wameahidi kuleta mabadiliko endapo wakipata nafasi ya kuingia madarakani.

Post a Comment