Beki na nahodha wa klabu ya Mbeya City, Juma Said Nyosso amesema
hakumbuki kama alimfanyia kitendo cha utovu wa nidhamu mshambuliaji na
nahodha wa klabu ya Azam FC John Bocco.
Nyosso, alisema hayo jana alipofanyiwa mahojiano na muandishi wa
habari za kituo cha Azam TV, ambapo alibainisha huenda kitendo hicho
kikawa kimetengenezwa kwa makusudi ya kumkandamiza, kutokana na makosa
aliyowahi kuyafanya siku za nyuma.
Kwa kuhofia jambo hilo, beki huyo ambaye aliwahi kuzitumikia klabu za
Ashanti Utd, Simba pamoja na Costal Union kabla ya kusajiliwa na Mbeya
City, ameutaka uongozi wa chama cha wachezaji wa soka SPUTANZA
kumsimamia na kumtetea katika sakata hilo ambalo limemuingiza kwenye
kifungo cha miaka miwili sambamba na kutozwa faini ya shilingi million
mbili.
“Sikumbuki kufanya hivyo, huenda watu wananihukumu kwa yale niliyofanya nyumba,” alisema.
Naye kocha mkuu wa Mbeya City, Juma mwambusi alisema amejaribu
kuufuatili mchezo wa Azam FC dhidi ya kikosi chake kwa njia ya
televisheni na kubaini hakukua na kosa kama hilo, hivyo ameziomba
mamlaka za soka kutenda haki dhidi ya Nyosso.
“Siung mkono vitendo vya utovu wa nidhamu kwa mchezaji wangu yoyote
anapokua ndani na nje ya uwanja, hivyo nitakua mpuuzi kama nitamtetea
Nyosso kwa kosa ambalo anadaiwa kulifanya, wakati mimi ni muumini wa
nidhamu siku zote” Alisema Juma Mwambusi.
Katika hatua nyingine Mwambusia meahidi kumtumia Juma Nyosso katika
mchezo wa hii leo dhidi ya Toto African utakaochezwa jijini Mwanza
kwenye uwanja wa CCM Kirumba, kwa madai hajapokea taarifa rasmi kutoka
bodi ya ligi.
Post a Comment