Shirika la umeme Tanzania -Tanesco limesema hali ni mbaya ya upatikanaji wa umeme nchini kutokana na chanzo kikuu ambacho ni maji kuzalisha nishati hiyo asilimia 18 tu ya uwezo wake na kwamba hali hiyo imewafanya washindwe kuita kukosekana huko umeme nchini kama ni mgawo au dharura.

Mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo Mhandisi Felchesm Mramba amesema makali ya tatizo hilo kwa kiasi fulani yamepunguzwa kutokana na kupatikana kwa nishati ya gesi ambapo pia jumanne ya wiki hii wamefanikiwa kuwasha megawati 30 kutoka kampuni ya Simbioni.

 

Post a Comment