Mgombea nafasi ya urais kwa tiketi ya Chadema anayeungwa mkono na vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA Edward Lowassa amesema serikali atakayoiunda itahakikisha inajikita katika kupambana na upatikanaji wa ajira nyingi zaidi kwa vijana hapa nchini.
Siku 11 pekee kabla ya sanduku la kura kuzungumza,
Lakini kwanza ni onyo kwa baadhi ya vigogo wa serikali.
 
Akiwa mjini Geita amehutubia mikutano mikubwa minne tofauti iliyohudhuliwa na idadi kubwa zaidi wa wananchi ambapo aliwahakikishia vijana wa kitanzania kuwa serikali yake itahakikisha ajira zaidi kwa vijana zinapatikana.
 
Mgombea huyo wa urais Edwrad Lowassa anayetajwa kama kiongozi mwenye ndoto ya Tanzania mpya amewahakikishia watanzania na wanageita kwa ujumla kutatua tatizo wachimbaji wadogo.
 
Comled Kingunge Ngombale Mwiru akihutubia maelfu ya wakazi wa mjini Geita licha ya kuwataka wanaobeza uamuzi wake wa kukitosa chama cha CCM, kuacha mara moja kumuandama na kutoa rai kwa watanzania.

 

Post a Comment