Mshambuliaji Radamel Falcao, hana nafasi kubwa ya kuendelea kukaa
Stamford Bridge yalipo makao makuu ya klabu ya Chelsea, kwani huenda
akaondoka mwezi januari mwaka 2016.
Mshambuliaji huyo kutoka nchini Colombia, alipewa nafasi kubwa ya
kuitumikia klabu hiyo ambayo inashikilia taji la ubingwa nchini England,
baada ya kusajiliwa mwanzoni mwa msimu huu, lakini imeonekana mambo
kumuendea tofauti chini ya utawala wa meneja Jose Mourinho.
Mpaka sasa Falcao ameshacheza michezo saba akiwa na klabu hiyo na
amefunga bao moja, hali ambayo imempotezea imani Mourinho pamoja na
mashabiki wa Chelsea, ambao waliamini wamepata mshambuliaji ambaye
angekua mbadala wa Didier Drogba aliyeondoka klabuni hapo mwishoni mwa
msimu uliopita.
Falcao, anapigiwa chapuo la kurejeshwa kwenye klabu yake ya AS Monaco
ambayo imekua ikimtoa kwa mkopo tangu msimu uliopita alipokwenda Man
Utd na sasa yupo Chelsea.
Akiwa Man Utd msimu uliopita, Falcao mwenye umri wa miaka 29, alicheza michezo 29 na kubahatika kufunga mabao 4 pekee.
Post a Comment