Mjumbe wa Kamati ya Kampeni ya CCM, January Makamba ameonesha kutokubaliana kwake na ripoti za kinachojili kwenye mikutano ya mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa na kueleza kuwa Magazeti hutumiwa kupiga kampeni.
Makamba ameeleza hayo kupitia mtandao wa Twitter baada ya
mtu mmoja anaetumia jina la ‘Gachanja Muigai’, kumueleza kuwa kutokana
na kile wananachokisoma, inaonekana kuwa wananchi wengi wanamuunga mkono
Lowassa. Na akataka kupata maoni ya Makamba kutokana na hali hiyo kama
anadhani wataweza kushinda.
“@JMakamba @MagufuliJP From what we
read here, it seems #Lowassa is resonating with Wananchi. Una hakika si
wakati wa kuvuka sakafu?” Aliuliza.
Makamba alimjibu kuwa
wapinzani wanatumia baadhi ya magazeti kama sehemu ya kampeni zao lakini
tafiti na hali halisi nchini inaeleza tofauti.
“They’ve turned
some newspapers into their campaign fliers. But the polls & mood
across Tanzania tell another story.”
Post a Comment