Chama cha soka nchini England FA, kimetoa taarifa za kutomchukulia
hatua zozote za kinidhamu meneja wa klabu ya
Chelsea, Jose Mourinho kufuatia sakata la aliyekua daktari wa kikosi cha
klabu hiyo, Eva Carneiro lililotokea mwanzoni mwa msimu huu.
FA, walikua wakifanya uchunguzi dhidi ya Mourinho, baada ya kuibuka
kwa tuhuma za unyanyasaji wa kijinsia, ambapo meneja huyo kutoka nchini
Ureno alidaiwa kuufanya wakati alipokua akimkalipia Eva Carneiro
alipoingia uwanjani kwenda kumpa huduma ya kwanza Eden Hazard.
Uchunguzi wa FA umeshindwa kudhihirisha ukweli wa maneno yaliyozungumzwa na Mourinho hivyo wameamua kuiweka pembeni kesi hiyo.
FA, walilazimika kufanya uchunguzi wa tuhuma hizo baada ya
kushawishiwa na vyombo vya habari ambavyo vilijitahidi kufuatilia kwa
ukaribu tukio hilo na vilibaini maneno ya unyanyasaji yaliyozungumzwa na
Mourinho kwa kuweka picha za televisheni kwenye mitandao.
Hata hivyo vyombo hivyo vya habari vilikwenda mbali zaidi, kwa
kuandika maneno ya unyanyazaji yaliyozungumzwa na Mourinho dhidi ya Eva
Carneiro wakati akiingia uwanjani na alipotoka.
Neno kubwa ambalo lilipewa nafasi ya kujadiliwa na kuandikwa na
vyombo vya habari vya nchini England, ni lile lililodhihirisha kumtusi
Eva Carneiro kwa kuitwa mtoto wa kahaba.
Eva Carneiro, ameshaondoka kwenye klabu ya Chelsea, na amekataa
kurudi kazini baada ya kutakiwa kufanya hivyo na viongozi wa klabu hiyo
huku akisistiza kusaka ushauri wa kisheria ili aweze kulifikisha suala
lake kwenye vyombo vya sheria kusaka haki dhidi ya Jose Mourinho.
Post a Comment