Aiba mtoto ili aolewe
Mwanadada Onyebuchi Jennifer,( 26 ) akitokea katika mji wa Anambra nchini Nigeria jumanne wiki hii amejikuta mikononi mwa polisi baada ya kukubali kwamba aliiba mtoto lakini si kwa nia ya kumdhuru.
“Ni kweli niliiba mtoto, na ningemrudisha mtoto huyo kwa wazazi wake baada ya kufanikiwa lengo langu la kufunga ndoa na mchumba wangu”, Jennifer aliwatonya mamwera hao.

Mchumba wa Jennifer ambaye jina lake halikuweza kufahamika mapema ,aliahidi kumuoa kimwana huyo endapo kama angemzalia mtoto kwanza. Kabla hajakutana na mchumba huyo, mnamo mwaka 2010 Jennifer aliwahi kufanikiwa kupata mtoto lakini baada ya siku kadhaa mtoto huyo alifariki.

Mwaka jana alikutana mchumba wake huyo ambaye aliahidi kuoana na Jennifer endapo kama angemzalia mtoto kwanza.
Akiwa na mchumba wake, Jeniffer aliweza kupata ujauzito lakini baada ya miezi mitatu ujauzito huo uliharibika. Jennifer anasema hakuweza kumwambia mchumba wake huyo hivyo akaamua kumficha.

Ili kuepuka msala wa kushtukiwa Jennifer aliamua kusafiri hadi mjni Logos na kusaka kazi, na alifanikiwa kupata kazi ya usaidizi kwenye kituo cha kuuza mafuta.
Wakati akiwa Logos, na miezi kadhaa kusonga ndipo hapo siku moja Jennifer akaamua kuzama super market kuzuga kama anaenda kununua bidhaa.
Onyebuchi-Jennifer-360x317
Huyu ndio Jennifer
Akiwa ndani ya Super Market hiyo alimuona mama mmoja mwenye mtoto, aliamua kumfuata na kuwa karibu naye.
Jennifer alimuomba Mama huyo ambebe mtoto wake kwani alivutiwa na mtoto wake, na bila hiana mama alitoa mtoto huyo.
Wakati wanaendelea kuzunguuka kwenye super market Jennifer alifanikiwa kuchomoka na mtoto huyo.
Jennifer aliondoka kabisa mjini logos na kurudi kwa mchumba wake huyo na kumueleza kwamba tayari amepata mtoto.
Baada ya siku nne Jennifer alikamatwa na polisi ambao walikuwa wakifanya uchunguzi mzito kumsaka aliyefanya tukio hilo.
Kesi inaendelea kufuatiliwa huku mchumba wa Jennifer akikataa tena mipango ya ndoa na kumuacha Jennifer akipambana na kesi hiyo.
The-baby-with-his-parents
Mtoto aliyewahi kuibiwa akiwa na Wazazi wake halisi
Jennifer ameomba msamaha kwa familia ya mtoto huyo na jamii kwa ujumla na kusema hayo ni majaribu aliyokutana nayo kwenye maisha yake lakini kama angefanikiwa kufunga ndoa basi angemwambia mume wake ukweli halisi na kisha angemrudisha mtoto huyo kwa Mama yake.

 

Post a Comment