Mgombea wa nafasi ya urais kupitia Chadema anayeungwa mkono na vyama
vinne vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA Edward Lowassa
ameingia mjini Monduli na kupata mapokezi makubwa huku akiahidi
kuendelea kushughulikia changamoto za kimaendeleo ndani ya jimbo hilo.
Tofauti na mawazo ya wengi, akiwa monduli kazi yake ya kwanza
aliyoifanya ni kumtangaza Bw Julius Kalanga kuwa mrithi wake wa kiti cha
ubunge jimbo la Monduli.
Mgombea huyo aliyekuwa mbunge wa jimbo la Monduli kwa kipindi cha
miaka 20, amewashukuru wakazi wa jimbo hilo kwa ushirikiano waliompatia
uliowezesha kupatiakana kwa maendeleo ndani ya jimbo hilo huku akiahidi
kuendelea kutekeleza ahadi ambazo bado hajazikamilisha.
Edwrad Lowassa ametumia jukwaa la mto wa mbu wilayani Monduli
kuwaomba watanzania kuhakikisha wanampigia kura nyingi zaidi kwani
uwezo, nia na sababu ya kuwa mshindi wa kiti cha urais anao.
Fredrick Sumaye amewataka wanamonduli na watanzania kwa ujumla
kuhakikisha wanaunga mkono kauli mbiu ya mabadiliko kwani umasikini wa
watanzania umechochewa na uongozi mbovu wa CCM kwani rasilimali nyingi
za nchi zimeshindwa kuwanufaisha watanzania.
Katika siku yake ya kwanza ya kampeni kanda ya kaskazini huku
akitumia usafiri wa chopa alifanikiwa kuhutubia maeneo ya, Mangora,
Mburu na mto wa mbu wilayani Monduli kabla ya kuhutubia maelfa ya wakazi
wa mjini Babati mkoani Manyara katika uwanja wa Kwaraa.
Post a Comment