Kiungo Michael Carrick anapewa nafasi kubwa ya kuwa sehemu ya kikosi cha Man Utd ambacho mwishoni mwa juma hili kitacheza mchezo wa ligi kuu ya soka nchini England, dhidi ya Arsenal kwenye uwanja wa Emirates.
Meneja wa Man Utd, Louis van Gaal amethibitisha kuwa katika harakati
za kumtumia kiungo huyo, kutokana na hali yake kuendelea vyema baada ya
kujiuguza maumivu ya misuli ya mwili kwa siku kadhaa zilizopita.
Van Gaal, amesema anajihisi mwenye furaha kuwa na matarajio ya
kumtumia kiungo huyo mwenye umri wa miaka 34 katika mchezo huo, na
anaamini uzoefu alionao utakisaidia kikosi chake kupambana vyema na
kuondoka na point ugenini.
Carrick, alikua nje ya kikosi kilichocheza mchezo wa ligi ya mabingwa
barani Ulaya siku ya jumatano dhidi ya Wolfsburg ambao walikubali
kufungwa mabao mawili kwa moja kwenye uwanja wa Old Trafford.
Post a Comment