Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini NEC imetakiwa iandae utaratibu
ambao utawasaidia wananchi wote waliojiandikisha kwenye vituo ambavyo
hawawezi kupiga kura waweze kupiga kwani ni haki yao ya msingi.
Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa Mtandao wa Asasi za kiraia wa
kuangalia chaguzi Tanzania, Bi Imelda Urio jana wakati akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Bi Uria amesema kuwa ipo haja kwa NEC kufanya baadhi ya marekebisho
katika changamoto kadhaa zilizojitokeza moja wapo ikiwa ni swala la
wanafunzi wa vyuo kutokuwa na sehemu ya haki ya kupiga kura ili
ifikifika oktoba 25 mapungufu hayo yasiweze kujitokeza na uchaguzi huo
ukawa wa huru na haki.
Aidha ameisihi serikali kutofanya mabadiliko tena ya watumishi kwenye
Tume hiyo ili kuondoa hali ya wanasiasa kutokuwa na imani na tume hiyo.
Post a Comment