Wanawake wa wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro wamekumbushwa  kuwa hatma ya kero za kukosa huduma mbalimbali zikiwemo huduma za afya ya uzazi ipo kwenye mikono yao ifikapo Octoba 25  kwa kuchagua viongozi waadilifu watakaoweka  maslahi mapana ya kero za wanawake mbele.

Mke wa mombea urais kupitia umoja wa vyama vinavyounda Ukawa mama Regina Lowassa ameyasema hayo wakati akizungumza na wanawake wa wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro ambapo amesema wanawake wanahitaji mabadiliko na hakuna sababu ya wanawake kuendele kubeba mizigo mizito ya michango kwenye maswala ya afya na elimu.

 

Post a Comment