Tume ya Taifa ya Uchaguzi yazindua kituo cha Mawasiliano cha huduma kwa Wateja

Jumla ya Simu 1,381 zimepokelewa katika kituo cha Mawasiliano cha Tume ya Taifa ya Uchaguzi – Nec Call Center, kilichoanzishwa mahususi kwa lengo la kuwasaidia wapiga kura pamoja na wadau mbalimbali wa uchaguzi ili kupata elimu ya mpiga kura.

Kupitia kituo hicho ambacho kimeanza rasmi oktoba 12 mwaka huu kinatumika kwa kuuliza maswali yanayohusu uchaguzi mkuu wa Urais, Ubunge na Udiwani, sanjari na kutoa ushauri na taarifa mbalimbali za vurugu zinazoweza kutokea wakati wa uchaguzi.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jana jijini Dar es salaama, Mkurugenzi wa Uchaguzi, Ramadhani Kalima ametaja inaayotakiwa kutumiwa na wananchi ni 0800782100 .

Kalima amesema namba hiyo itakuwa hewani kuanzia oktoba 12 – 18, kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni. Lakini kuanzia oktoba 19 – 30 namba hiyo itakuwa ikitumika saa 24 na itakuwa ni bure.

Post a Comment