![](http://i1.wp.com/millardayo.com/wp-content/uploads/2015/10/obaa.jpg?resize=600%2C337)
Hivi karibuni rapper wa Marekani Kanye West alitangaza nia yake ya kutaka kuingia ikulu ya Marekani katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka 2020.
Kanye alitangaza nia yake hiyo wakati wa tuzo za VMAs 2015.
Rais wa Marekani Barack Obama amemshauri
rapper huyo kuhusu uamuzi wake huo wakati wa alipohudhuria hafla ya
uchangishaji fedha huko San Francisco iliyofanyika jana Oktoba 10 wakati
Kanye West naye akiwa mmoja wa waliohudhuria.
Kwanza Obama alishangazwa na uamuzi wa Kanye West kuwania nafasi hiyo
na pia hakuwa na kikubwa cha kumshauri kuhusu uamuzi wake huo.
Amemtaka kama Rais atumie muda mwingi kufanya maamuzi kwa sababu kuna
watu wengi ambao wana tabia za ajabu hivyo anapaswa kukabaliana nao ili
aweze kumudu nafasi yake.
Pia alimuuliza kama anafikiri tena Wamarekani watampa Mmarekani mweusi nafasi ya kuwaongoza kama ilivyokuwa kwake.
Obama na Kanye West wote wametokea katika jimbo la Chicago Kusini.
Post a Comment