Wanasayansi wazindua Mfumo mpya wa Taarifa za Matokeo ya Mwanafunzi Shuleni kumfika Mzazi moja kwa moja

Baadhi ya vikundi vilivyopo kwenye sekta ya sayansi hapa nchini vimegundua mfumo mpya wa utoaji taarifa za matokeo ya mitihani unaotarajiwa kuzinduliwa oktoba 8 mwaka huu kwa wanafunzi wa shule za sekondari ili yaweze kumfikia mzazi kwa wakati kupitia simu ya mkononi.

Akizungumza na radio Times Fm, Mkuu wa kitengo cha Ubunifu kiitwacho Edu Taarifa katiaka idara ya Sayansi, Mile Hassan amesema kuwa mfumo huo utamuwezesha mzazi kufahamu mwenendo wa mtoto wake kitaaluma pamoja na kupata taarifa muhimu za uongozi wa shule husika.

Ameongeza kuwa mpango huo utapunguza tabia ya utoro kwa wanafunzi na kuongeza maadili kwa mtoto pindi Mzazi anapogundua maendeleo hayo.
Mfumo huo utahusisha matokeo ya mtihani na majaribio mbalimbali yanayofanyika kwa kipindi cha mwezi na wiki na si mitihani ya Taifa.

 

Post a Comment