Chama cha NCCR Mageuzi chamsimamisha Kazi Makamu Mwenyekiti

Chama cha NCCR Mageuzi kimemsimamisha kazi Makamu Mwenyekiti wake Bara Mama Leticia Mosore kutokana na madai kwamba amekiuka Katiba ya Chama hicho kuwa kumshtumu Mwenyekiti wake Tiafa James Mbatia kwamba anakihujumu chama.

Hatua ya kumsimamisha imefikiwa septemba 22 mwaka huu, kwa taarifa ya maneno bila kumpatatia barua kwa lengo la kuendelea kufanya uchunguzi juu ya malalamiko yaliyotolewa na Mama Mosore.
Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa NCCR Taifa Mh. James Mbatia ameelezea hatua hiyo iliyochukuliwa.

James Mbatia amesema Makamu Mwenyekiti huyo alishirikiana na kundi la wanachama wengine kutunga taarifa za uzushi na kutumiwa na baadhi ya watu wasiopenda maendeleo ya chama cha NCCR.

Post a Comment