Mgombea urais  kupitia chama cha chadema anayeungwa mkono na vyama vinne vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi ukawa Edward Lowasa  ameahidi kuboresha mishahara ya walimu na kulipa stahiki zao zote kama watanzania watampa ridhaa kuwa rais wa nchi.
Baada ya kuhitimisha kwa kishindo kanda ya kaskazini sasa ni rasmi   kanda ya ziwa akianzia tarime mkoani Mara.
 
Edward Lowasa anayetajwa kama mkombozi wa tanzania ijayo, amesema ni dhamira yake kuona mtanzania akineemeka na keki ya taifa huku suala la elimu kwake akisema ndio itakuwa slaha kubwa ya kuifikisha Tanzania panapotakikana.
 
Fredric Sumaye  waziri mkuu mstaaf amesema wanatarime na watanzania kwa ujumla hawanabudi kuitumia vema Oct 25 kwa kukiondosha chama cha CCM kwani kuna kila dalili ya kuchokwa na watanzania.
 
Akiwa mjini tarime Edward Lowasa alifanikiwa kuhutubia mikutano katika maeneo yasalali,nyamongo na mgumu kabla ya kuhitimisha kwa kuhutubia maelf ya wakazi wa mji wa tarime katika uwanja wa sabasaba.

 

Post a Comment