Tume ya taifa ya uchaguzi imewataka mawakala na jeshi la polisi nchni kuhakikisha wanatenda haki kwa vyama vyote wakati wa wananchi kupiga kura ili kuepuka malalamiko yanayoweza kusababisha uvunjifu wa amani katika vituo vya kupigia kura.

Akizungumza na wasimamizi wa uchaguzi wa nchni nzima na jeshi la polisi nchni, mnweyekito wa tume ya taifa ya uchaguzi-NEC- jaji mstaafu Damiani Lubuva amewataka watendaji hao kufuata sheria na kanuni za tume na kuwataka kutambua kuwa mapungufu madogo yanaweza kusababisha  uvunjifu wa amani. 
 
Kutokana na baadhi ya vyama vya siasa za kuwataka wapiga kura kubaki katika vituo baada ya kupiga kura jaji Lubuva amewaagiza wasimamizi wa uchaguzi na jeshi la polisi nchni kutoruhusu watu kusubiri matokeo ya uchaguzi katika eneo la kupiga kura kwa kisingizia cha kulinda kura.

 

Post a Comment