Asilimia kubwa ya  watoto  wanaotoka  katika  familia  maskini   wilayani  Longido mkoani Arusha  wanashindwa  kuhudhuria  masomo  kutokana  na changamoto zinazowakabili  wazazi  wao likiwemo  tatizo  la njaa,ukosefu wa huduma ya maji,na Afya. 

Wakizungumza wakati wanapokea msaada wa zaidi ya milioni  230  zilizotolewa na mfuko wa Tassaf baadhi ya wananchi wa vijiji vinavyokabiliwa na matatizo hayo pamoja  na  kuushukuru  mfuko wa  Tasafu  wamesema  ukosefu wa huduma  za kijamii bado  ni janga   kubwa  kwao na watoto wao.
Baadhi ya viongozi wamesema pamoja  na  kusisitiza  wazazi  kupeleka watoto  wao shule wanatembea  umbali mrefu  na wanapofika  shule  wanasinzia badala  ya  kumsikiliza  mwalimu  na jambo  lililoko wazi  kuwa  hawataweza kufanya vizuri.
 
Wakikabidhi  fedha hizo  mkurugenzi  wa halmashauri  ya  wilaya  ya  longido  bw.Felexs Kimario na watendaji  wa Tasaff  wamesema  vijiji  27  vimefikiwa  na  mpango  huo na kaya 259  zimepatiwa  msaada  huo  ambao ni  kwa ajili  ya kusaidia elimu afya na kujikimu.
 
Longido ni miongoni  mwa wilaya za  mkoa wa Arusha  zinazokabiliwa  na tatizo  kubwa  la  ukosefu  wa huduma  za  kijamii  ikiwemo  maji,miundombinu  ya  elimu na Afya.
 

Post a Comment