WASHITAKIWA nane wamefikishwa mahakani kwa kosa la jinai ya kukusanya matokeo ya uchaguzi Mkuu wa Urais mwaka huu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kuyachapisha kupitia mitandao ya kijamii bila ya kuihusisha tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Washitakiwa
hao, Mashinda Edwin Mtei (45),Mkazi wa Tengeru-Arusha, Julius Mwita
(30), Mkazi wa Magomeni-Dar es Salaam, Frederick Eddie Fussi (25), Mkazi
wa Mbezi beach-Dar es Salaam, Meshack Carlos Mlawa (27), Mkazi wa
Keko-Dar es Salaam, Anisa Nicholas Rulanyaga (41), Mkazi wa Kawe-Dar es
Salaam, Jose Mavinga Nimi(51), Mkazi wa Paris-Ufaransa, Julius Mwonga
Matei (45), Mkazi wa Mwangazi-Kitui, Kenya na Kim Hyunwook (42) wa
Busan-Korea Kusini.
Ilidaiwa
mahakamani hapo kuwa tukio hilo litokea kati ya Oktoba 25 na 26 mwaka
huu katika maeneo tofauti ya jiji la Dar es Salaam, kupitia mtandao wa
kitaifa wa usimamizi wa uchaguzi uliopewa jina la “Mfumo wa usimamizi wa
matokeo ya uchaguzi wa M4C” (M4C National Results management system) na
mitandao mengine ya kijamii ya Facebook na Twitter.
Mahakama
ya Kisutu imesikiliza kesi hiyo mbele ya hakimu mkazi kisutu, Respicius
Mwijage baada ya kufahamika kuwa data za watuhumiwa hao zilizowekwa
mitandaoni hazikuwa sahihi na hazikuwa na ukweli wowote, yanayodaiwa
kupotosha umma juu ya matokeo yanayoendelea kutolewa na Tume ya Taifa ya
Uchaguzi.
Makosa
mengine kwa washitakiwa no.4, 7 na 8, ambao ni Julius Mwonga Matei,
Jose Mavinga Nimi na Kim Hyunwook wanatuhumiwa kujihusisha na ajira bila
kibali siku ya Oktoba 26 wakiwa katika hotel ya King D iliyopo wilaya
ya kinondoni wakiwa na vitambulisho vya uraia wa Kenya, Angora na Korea,
vyenye No. A.1532119, 30879 na M.27687807 wakishiriki katika ajira ya
kukusanya na kuchapisha matokeo ya uchaguzi wa Rais kwa CHADEMA bila ya
uhalali wa kibali.
Mahakama
inawashitaki kwa tukio hilo lililodaiwa kwenda kinyume na kifungu cha
16(1) na 31(1)(m) cha sheria ya uhamiaji ya mwaka 2002 ambayo ni sawa na
Sheria No.8 iliyofanyiwa marekebisho mwaka huu.
Kosa
lingine la mshitakiwa no.4, Julius Mwonga, ni kujihusisha katika
biashara kwa niaba ya WANAMA SACCOS bila ya kibali akiwa na kitambulisho
chake cha uraia wa Kenya chenye No.A.1532119.
Mshitakiwa
anashitakiwa kwa kwenda kinyume na kifungu cha 16(2) na 31(1) cha
sheria ya uhamiaji ya mwaka 2002 ambayo ni sawa na Sheria No.8
iliyofanyiwa marekebisho mwaka huu.
Mahakama
imetoa tarehe ya kuamua kutoa au kutotoa dhamana kwa watuhumiwa hao
hadi Oktoba 30 mwaka huu, ambapo kwa upande wa watuhumiwa kesi hiyo
inasimamiwa na mawakili wawili, Peter Kibatala na Omary Msemo ambao
wamempinga mwanasheria wa Serikali dhidi ya kuitaka mahakama itoe
dhamana kwa watuhumiwa hao.
Post a Comment