Rais Jakaya Kikwete jana amezindua rasmi kituo cha kufua umeme
kilichopo kinyerezi jijni Dar es Salaam hatua ambayo inaashiria mgao wa
umeme nchini kuanza kupungua siku hadi siku.
Akizindua kituo hicho, Rais Kikwete amesema kuwa uamuzi huo unaenda
sambamba na mpango mpya ambao unatarajia kuanza mwakani utakaoibua fursa
za uchumi wa maendeleo kwa watanzania baada ya kunufaika kwa kuwa na
umeme wa uhakika.
Aidha Rais Kikwete amebainisha kuwa hadi sasa vyanzo vyote vilivyopo
vya umeme wa maji havijaweza kufikisha kiasi kinachotakiwa kusambaza
umeme nchi nzima hivyo kwa hatua hiyo ya kuanza kutumia umeme wa gesi
kutarahisisha ugawaji wa umeme sehemu mbalimbali nchini.
Hata hivyo Rais Kikwete ameendelea kusema kuwa katika mipango ya
maendeleo inayotekelezwa hivi sasa ya miaka mitano ambayo inaisha mwaka
ujao lengo lilikuwa ni kufikisha umeme wa megawatts 2780 ambapo amesema
kuwa bado jitihada zinafanyika ili mwaka ujao wafikie malengo hayo.
Post a Comment