Mwanasiasa Mkongwe  Kingunge Ngombare Mwiru leo ametangaza kujiondoa ndani ya Chama cha Mapinduzi CCM na sasa atakuwa mwananchi huru.
Kingunge amezungumza mbele ya waandishi wa Habari leo akiwa nyumbani kwake Kijitonyama, Dar es salaam.
Amesema kutokana na matukio yaliyotokea katika kumpata mgombea Urais ni tofauti na ilivyokuwa mwaka 1995 na 2005 hivyo kuamua kuondoka ndani ya chama hicho.
Amesema hawezi kuhimili chama kisichojiendesha bila katiba na anajua uamuzi wake utawasumbua baadhi ya ndugu zake, wazee na makada wengine.
Amesema kwa sasa hakusudii kujiunga na chama kingine chochote kwa kuwa amekuwa mwanaharakati kwa miaka 61.

Post a Comment