![Van Gaal: Niliwaambia Wawe Makini Dakika Za Mwanzo](http://www.timesfm.co.tz/wp-content/uploads/2015/10/VAn-G-559x520.jpg)
Ushindi wa mabao matatu kwa sifuri uliowapa Arsenal point tatu
nyumbani, umeshindwa kumpa nafasi meneja wa klabu ya Man Utd, Louis van
Gaal kuzungumza kwa busara mbele ya vyombo vya habari na badala yake
alijikuta akibwatuka.
Van Gaal, alionyesha hasira za kupoteza mchezo wa jana jioni kwa kusema kikosi chake kilikua dhaifu na mpaka alishindwa kukipachika jina la kushindwa kufanya vizuri kutokana na kukosa namna ya kufanya hivyo.
Van Gaal, alionyesha hasira za kupoteza mchezo wa jana jioni kwa kusema kikosi chake kilikua dhaifu na mpaka alishindwa kukipachika jina la kushindwa kufanya vizuri kutokana na kukosa namna ya kufanya hivyo.
Van Gaal alisema haikuwa matarajio yake kuona wachezaji wa Man Utd
wakicheza hovyo na kuruhusu mabao matatu ndani ya dakika 20 za kipindi
cha kwanza, hali ambayo anaiona kama anguko kubwa katika mipango
aliyokua amedhamiria itumike kwenye mchezo huo uliochezwa katika uwanja
wa Emirates.
Alisema ilikua ni vigumu kwao kuondoka na point tatu kwenye uwanja wa
ugenini kutokana na kuanza vibaya mchezo huo, hali ambayo iliwapa
nafasi Arsenal kutakata na kujipatia mabao ya haraka ambayo yalidumu
hadi dakika 90 zilipokamilika.
Hata hivyo meneja huyo kutoka nchini Uholanzi aliahidi kulitafutia
ufumbuzi tatizo lililojitokeza jana jioni kwa kuutumia muda wa juma moja
na nusu ambapo wachezaji watakua na timu zao za taifa na watakaporejea
shughuli ya kurekebisha makossa itaanza rasmi.
Lakini pamoja na kulalamika huko, Van Gaal amewapongeza Arsenal kwa
kusisitiza walicheza vizuri na walizitumia vyema nafasi walizozipata.
Kufungwa katika mchezo wa jana, kumeifanya Man Utd kuporomoka kwa
nafasi moja kwa tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa huku wakiwa
sawa na Arsenal katika upande wa point.
Post a Comment