Aliyekuwa
mkurugenzi mtendaji wa shirika la reli Tanzania (TRL), Kipallo Kisamfu
na wenzake 10 wamefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu
wakikabiliwa na mashiataka tisa yakiwemo ya matumizi mabaya ya madaraka
kwa kupitisha ununuzi wa mabehewa mabovu 25.
Watuhumiwa hao pia kwa mujibu wa hati ya mashitaka wanadaiwa
kupitisha malipo ya zaidi ya shilingi bilioni 2.8 kinyume na taratibu.
Washtakiwa hao walisomewa mashitaka yao mbele ya hakimu mkazi
mwandamizi, Emmilius Mchauru. Huku upande wa jamhuri uoliongozwa na
mawakili wa serikali waandamizi, Shadrack Kimaro, Theophil Mutakyawa na
waendesha mashitaka wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa
(Takukuru), Max Ally na Maghela Ndimbo.
Max alidai katika shitaka la kwanza, kati ya februari mosi, 2013 na
juni 30, 2014 makao makuu ya TRL, mshtakiwa Kisamfu akiwa mkurugenzi
mtendaji kwa nia ovu alitumia vibaya nafasi yake kwa kushindwa kusimamia
zabuni na kusababisha kampuni ya M/S Hindusthan Engineering and
Industries Limited kupata faida.
Shitaka la pili linamkabili mshtakiwa wa sita, Mafikiri, ambaye
ilidaiwa kuwa kati ya julai mosi na agosti 31, mwaka 2013, makao makuu
ya TRL, akiwa fundi mkuu, alitumia vibaya madaraka yake kwa kupitisha
ramani ya mabehewa iliyoandaliwa kinyume cha sheria na kuisababishia
kampuni ya m/s hindusthan engineering and industries limited kupata
faida.
Max aliendelea kudai kuwa kati ya januari mosi na februari 28,
mwaka 2014 makao makuu ya TRL, akiwa kaimu mkuu wa ufundi, aliidhinisha
kampuni ya M/S Hindusthan Engineering and Industries Limited kufanya
ukarabati wa mabehewa 25 bila kujiridhisha na maombi ya tenda hiyo.
Katika shitaka jingine, ilidaiwa kuwa kati ya januari mosi na
februari 28, mwaka 2013, TRL, mshtakiwa wa nne, saba, nane, tisa na 10,
wakiwa wajumbe wa kamati ya kutathmini zabuni walitumia madaraka yao
vibaya kwa kupitisha kampuni ya M/S Hindusthan Engineering and
Industries Limited kufanya ukarabati huo na kuisbabishia kupata faida.
Washtakiwa walikana mashitaka yao. Upande wa jamhuri ulidai kuwa
upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na haukuwa na pingamizi la
dhamana.
Hata hivyo, mshtakiwa wa kwanza, tatu, nne na wa 11 walitimiza masharti hayo na kesi hiyo itatajwa februari 25, mwaka huu.
Washtakiwawaliopandishwa kizimbani ni pamoja na Jasper Kisiraga,
Mathias Massae, Muungano Kaupunda, Ngoso Ngosomwiles, Paschal Mafikiri,
Kedmon Mapunda, Felix Kashaigili, Lowland Simtengu, Joseph Syaizyagi na
Charles Ndenge.
Post a Comment