Ukosefu wa mazoezi kwa wale walio na umri wa kadri huzeesha akili na mwili ,utafiti umesema.
Ukosefu wa mazoezi kwa watu walio na umri wa miaka 40 uhusishwa na ubongo wenye ukubwa wa 60,kulingana na utafiti nchini Marekani.
Zoezi miongoni mwa watu wenye umri wa kadri ni muhimu hususan kwa watu wenye ishara za mapema za ugonjwa wa moyo,wamesema watafiti katika chuo kikuu cha Boston.

Utafiti huo pia umeongezea ukuaji wa ushahidi kwamba afya ya moyo huathiri afya ya ubongo katika maisha ya mbeleni.
Utafiti huo uliochapishwa katika jarida la matibabu katika chuo cha navu nchini Marekani,uliwahoji watu 1,583 walio na miaka 40.
Walioshiriki ambao hawakuwa na tatizo la akili ama hata ugonjwa wa moyo ,walijipima katika mashine ya kukimbia ,na kufanya hivyo tena baada ya miongo miwili pamoja na ukaguzi wa Ubongo.
''Tulibaini uhusiano wa karibu katika utafiti wetu kati ya wale wasiofanya zoezi na ukubwa wa ubongo miongo kadhaa baadaye,ambayo huonyesha ubongo ukizeeka'',alisema kiongozi wa utafiti huo Nicole Sarpatano kutoka chuo kikuu cha matibabu cha Boston.

Post a Comment