Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye amewasimamisha kazi watumishi wawili wa Shirika la Utangazaji la Taifa TBC kutokana na utendaji usioridhisha.
Akizungumza
na waandishi wa habari katika ofisi za TBC leo jijini Dar es Salaam,
Waziri Nape amewataja watumishi waliosimamishwa kazi kuwa ni Mkurugenzi
wa Idara ya Habari na Matukio Bwana Mbwilo Kitujime na Meneja wa Vipindi
Bibi. Edna Rajab ambao wote kwa pamoja wasimamishwa kazi na uamuzi huo
utafikishwa kwa Bodi ya TBC kwa hatua zaidi.
“Tunachukua
uamuzi wa kuwasimamisha kazi watendaji hawa ili kujenga upya Idara hii
muhimu katika ustawi wa TBC na habari kwa ujumla” Alisema Nape
Aidha
Waziri huyo amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa TBC kuwachukulia hatua
watumishi wengine walio chini ya Idara hiyo kwakuwa wako chini ya
mamlaka yake na kutoa mrejesho wa hatua alizochukua dhidi ya wale wote
wilioonyesha utendaji mbovu.
Alisema
kuwa Serikali imefikia uamuzi huo kutokana na kuwepo kwa malalamiko ya
muda mrefu juu ya utendaji mbovu na wakutoridhisha viongzi na baadhi ya
watumishi wa Idara hiyo hiyvo hatua hizo zimechukuliwa ikiwa ni kujenga
upya na kuboresha Idara hiyo muhimu katika uendeshaji wa Shirika lolote
lile la Habari na kuongeza ufanisi.
Idara
ya Habari na Matukio ya TBC inaundwa na Mkurugenzi wa Idara, Meneja wa
Vipindi Wahariri na Waandishi wa Habari ambapo tayari Mkurugenzi na
Meneja wa Vipindi wamesimamishwa kazi leo tarehe 15 Februari 2016 na
watumishi wengine watachukuliwa hatua kufuatia agizo la Mhe. Waziri wa
Habari kwa Mkurugenzi Mkuu wa TBC alilolitoa leo wakati akitangaza
kuwasimamisha kazi viongozi hao.
Post a Comment