Staa wa Bongo Fleva, Ali Kiba, mwezi ujao anatarajiwa kukwea pipa
hadi nchini Nigeria kwa ajili ya kufanya kazi na mwanamuziki wa nchi
hiyo, Deborah Oluwaseyi ‘Seyi Shay’.
Msanii huyo anayetamba na kibao cha ‘Right Now’, aliwaambia waandishi
wa habari jambo hilo wakati alipokuwa akizungumzia ziara yake ya kikazi
nchini Tanzania.
“Kwa Tanzania namkubali sana Ali Kiba na Christian Bella,” alisema
Seyi Shay. “Nimezungumza na Ali Kiba na kukubaliana tufanye kazi pamoja,
anatarajiwa kuja Nigeria, Machi mwaka huu kwa ajili ya kukamilisha
mchakato huo.”
Seyi Shay ni balozi wa Pepsi nchini Nigeria na alikuja Tanzania kwa
mwaliko rasmi wa kampuni hiyo nchini na alifanya shoo moja mkoani Mwanza
kabla ya kutembelea kiwanda cha Pepsi jijini Dar es Salaam kisha kurudi
nchini kwao.
Post a Comment