Chege:Napiga Stori na mwanangu kama tupo umri mmoja.

Msanii anayefanya vizuri katika muziki wa BongoFleva nchini Said Chege, ”Chege” amesema kuwa huwa anajisikia vyema kipindi anapokuwa na mwanaye aliyempata akiwa katika harakati za ujana.

Chege amefunguka kuwa hali ya yeye kupata mtoto ujanani inamfanya ajisiki raha kwani kwa sasa mtoto wake huyo yupo katika hatua ya elimu ya Sekondari
 
Huwa najisikia poa saana ninapokuwa karibu na mwanangu huwa tinapoga stori kibao kama tupo umri mmoja,alisema,

Chege alisema mtoto wake huyo anayeishi Mwanza amekuwa akija kumtembelea mara kwa mara Dar es salaam na kwamba amekuwa akijivuna na kujisikia faraja kwa kuwa na mtoto mwenye umri huo katika maisha ya sasa.

Post a Comment