WAZIRI
nchi ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mtaa,George
Simbachawane amewasimamisha kazi wakurugenzi wa nne kwa tuhuma za kuwahonga
wakaguzi wa fedha kutoka katika ofisi ya Mkaguzi mkuu wa Hesabu za
serikali (CAG) ili wapewe hati safi huku Halmashauri hizi zikiwa na
ufisadi .
Wakurugenzi waliosimamishwa kazi ni
Elizabeth Chitundu wa Halmashauri za Misenyi mkaoni Kagera, Ally
Kisengi wa Halmashauri ya Nanyumbu mkaoni Mtwara na Abdalla Mfaume wa
Halmashauri ya Mbogwe mkoani Geita.
Pia,Waziri
Simbachawene amemsimamisha kazi mkurugenzi Halmashauri ya Tunduma
Mkoani Mbeya Bi Halima Ajali ili kupisha uchunguzi kutokana matumizi
mabaya ya madaraka ikiwa ni pamoja na kuwatumia watoto wake katika
shuguli za halmashauri na kuwalipa posho na kusababisha upotevu wa
mapato.
Aidha,
Waziri Simbachawane pia ameziagiza mamlaka husika kuwasimisha kazi
watendaji wa ofisi ya mkaguzi wa Hesabu za Serikali nchini,CAG
waliohusika kupokea rushwa kutoka kwa wakurugenzi hao ili watoe hati
safi kwenye Halmashauri hizo huku zikiwa na ubadilifu wa fedha za Umma.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo mchana Jijini Dar es Salaam,Waziri
Simbachawene amesema Wakurugenzi hao wamegundulika baada ya uchunguzi
wa kina uliofanywa na wizara yake
Akibainisha
makosa ya kila mkurugenzi,Waziri Simbachawene amesema Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Misenyi, Bi Chitundu alimwagiza mweka hazina wake
Majaliwa Bikwato atoe rushwa ya Milioni tatu kwa maafisa wa ofisi ya CAG
kwa lengo la kuficha kasoro walizoziabini katika ukaguzi huo huku
akijua ni kosa kisheria. Watumishi wa wa ofisi ya CAG waliopokea pesa
hizo ni Stevin Buawa,John Elias pamoja na Kilembi Mkole
Katika
Halmashauri ya Nanyumbu, Simbachawene amesema kuwa tarehe 26 Juni
2015, mkurugenzi wake bwana Kasengi pamoja na mweka hazina Pasco Malowo
na mwasibu Emmanuel Mugesa walimkabidhi fedha Milioni 3 na laki tano
afisa wa ofisi ya CAG kwa lengo la kutoa hati safi
Waziri Simbachawene amesema mwezi Novemba mwaka jana , Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbogwe mkoani Geita Abdalla Mfaume na mweka hazina wake waliwapatia milioni 16 maafisa wakaguzi wa ofisi ya CAG ili wafiche ufisadi walioubaini
Amesema
katika Halmashauri hiyo pia kumegundulika kuwepo na ufisadi mkubwa
ikiwemo malipo ya mishahara hewa pamoja na malipo ya milioni 200
yaliotolewa pasipo kuwa na Stakabadhi
Post a Comment