Hanscana: Q chief tuache new generation tufanye yetu, tunamwaka mmoja ndani ya ‘game’ tuna drive na tunaishi vizuri.

Muongozaji wa video nchini Hanscana, amemjibu Q Chief kuhusu tuhuma
alizowarushia directors wa video wa bongo kwamba hawana lolote na hawezi
fanya nao kazi tena.

“Ye ana stress za maisha, haiwezekani ukafanya muziki zaidi ya miaka 17
halafu huna hata pikipiki wakati kuna watoto wamekuja tu juzi kirahisi
rahisi alafu wana kila kitu,” alisema Hanscana.

“Kwa hiyo lazima upate mastress uanze kutapatapa, si unajua mfa maji, u
can see ur self jamaa ana more than 17 yrs in the game alafu he got
nothing, halafu kuna watoto tu wadogo wanafanya kitu, kwa hiyo unaweza
ukafikiria, suala dogo kama hilo kitaalamu hizo ni stress za maisha,”
aliongeza Hanscana.

Pia Hanscana amemtaka Q Chief akae pembeni na kuwaachia wasanii wachanga
wafanye kazi kwa sasa, na yeye abaki kuwa mtazamaji.
“Ninachomshauri atuachie tu new generation tufanye vitu vyetu , tuna
mwaka mmoja ndani ya game tuna drive, tunaishi vizuri, atuache tu vijana
aangalie tu game awe anatuangalia Youtube,” alisema Hanscana.

Post a Comment