Licha ya stori nyingi kuandikwa kwa namna tofauti kuhusu Jose Mournho, lakini ukweli au lengo na maana ya hizo habari nyingi huwa ni kuhusu Jose Mourinho kuchukua nafasi ya Louis van Gaal Man United, lakini kocha Louis van Gaal ana mtazamo tofauti kidogo na magazeti na wengi wanavyoamini, kuhusu Mourinho kujiunga na Man United.

Vyombo vingi vya habari hususani vya Uingereza vinaamini na vimeandika kuwa Jose Mourinho atamrithi Louis van Gaal mwishoni mwa msimu huu wa 2015/2016, kwani viongozi wa Man United hawajaridhishwa na mwenendo wa timu yao, hivyo wanataka kufanya mabadiliko ya kocha mwishoni mwa msimu.
103373911-476844

Lakini Louis van Gaal yeye haamini kuwa Jose Mourinho atajiunga na Man United ila anachojua yeye ni kuwa Man United hawajafanya mazungumzo yoyote na Jose Mourinho ” Mourinho ni rafiki yangu, lakini sijui kama Man United wamezungumza na Mourinho au la, ninachoweza kusema ni kuwa nimezungumza na mtendaji mkuu wa Man United Ed Woodward, lakini huwezi kufikiri kama wamefanya mazungumzo wawili hao, ninachofikiria ni kuwa Man United wamefanya mazungumzo na kocha mwingine” >>>> Van Gaal

Post a Comment