Mgombea
urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif
Hamad, ameithibitishia rasmi Tume ya Uchaguzi Zanzibar (Zec) kujiondoa
kuwania wadhifa huo katika Uchaguzi wa marudio utakaofanyika Machi 20,
mwaka huu.
Mbali
na Maalim Seif, wagombea wote wa chama hicho wa nafasi ya Uwakilishi na
Udiwani wamejiondoa kwa kuwasilisha barua rasmi kuwa hawatoshiriki
uchaguzi huo wa marudio wa Zanzibar.
Mkurugenzi
wa Mipango na Uchaguzi wa CUF, Omar Ali Shehe, amesema Maalim Seif
amewasilisha waraka wa barua wa kujiondoa kwa Zec, Febuari 8, mwaka huu.
Amesema
hatua aliyochukuwa mgombea huyo ni utekelezaji wa wa azimio la Baraza
Kuu la Uongozi la Taifa la CUF kutoshiriki uchaguzi mkuu wa marudio
visiwani hapa.
Shehe
alisema kuwa Zec imetakiwa kutotumia jina wala picha za Maalim Seif na
taarifa zozote katika karatasi za wapigakura kabla ya kufanyika
uchaguzi huo.
Alisema
kuwa katika Barua yake Maalim seif amesisitiza kuwa uchaguzi wa Oktoba
25 mwaka jana ulikuwa uchaguzi huru na wa haki na Mwenyekiti wa tume ya
Uchaguzi ya Zanzibar Jecha salim Jecha hakuwa na mamlaka ya Kikatiba na
sheria kufuta matokeo ya Uchaguzi huo.
Hata
hivyo Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Salum Kassim alisema jana
kuwa ni mapema kueleza vyama vingapi vimekamilisha kuthibitisha
wagombea wake kama wapo hai na watashiriki uchaguzi kabla ya kufanyika
Machi 20, mwaka huu.
Post a Comment