Wasomi na wananchi wa kada mbalimbali wamesema ndani ya siku 100 za kwanza za rais John Magufuli zimewezesha kugusa maisha yao hasa kwa kuboresha huduma za kijamii.

Huku akiwa na ndoto ya kuijenga Tanzania mpya yenye viwanda wasomi na wachambuzi wa masuala ya uchumi nchini wanasema rais amefanikiwa katika suala la ukusanyaji wa kodi huku akivuka lengo kutoka bilioni 900 hadi kufikia trioni 1.4 kwa mwezi.
 
Rais pia anatajwa kuimarisha amani ya nchi kwa siku 100 huku pia democrasia ikitajwa kuimarika vema ambapo kwa mujibu wa Dkt James Jesse mhadhili kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam anasema rais hanabudi kuahkikisha  anashughulikia pia suala la Zanzibar.
 
Lakini maafisa kutoka bohari ya dawa Tanzania MSD wanasema mpaka sasa wamekwisha kuwafikia watanzania wengi zaidi katika mikoa tofauti huku wakiwahakikishai kuwa bei ni rafiki kwa kila mtanzania.
 
Wachambuzi pia wanasema miongoni mwa mafanikio makubwa katika huduma za kijamii ni ufanikishaji wa utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wengi zaidi wa elimu ya juu tofauti na miaka mingi iliyopita.
 

Post a Comment