Kama ulikuwa ni msiba wa ‘penzi’ basi
arobaini imeisha na sasa maisha yanaendelea kwa wasanii wa Bongo fleva,
Shilole na Nuh Mziwanda ambao uhusiano wao umekufa na kuzikwa kabisa.
Wiki chache baada ya couple ya
‘shiwanda’ kuvunjika, na juhudi za wadau mbalimbali kutaka kuwapatanisha
kugonga mwamba (soma hapa), inavyoonekana Nuh na Shishi kila mmoja
ameamua kuendelea na maisha yake kwa kufungua ukurasa mpya wa mapenzi
tena kwa vitabu tofauti.
Nedy Music
Shishi ndiye aliyeanza kuonesha dalili
za kumpata mrithi wa Nuh, kwa kuanza kupost picha za msanii anayetumia
jina la Nedy Music kwenye Instagram, na msanii huyo pia kupost picha
tofauti tofauti za Shishi kwenye ukurasa wake.
Siku ya Valentine wawili hao walizidi kuthibitisha tetesi za uhusiano mpya kwa kupost picha wakiwa kimahaba zaidi kwenye kochi.
Upande wa Nuh Mziwanda naye ameanza
kupost picha za msichana mwingine mrembo anayetumia jina la Erah Erah
kwenye Instagram, ikiwa ni pamoja na picha walizopiga pamoja kama
couple, na mrembo huyo kupost pia kwenye ukurasa wake.
Erah Erah
Picha zingine zikimuonesha Nuh akiwa amelala na mikono ya mrembo huyo ikimpapasa usoni.
Hali hiyo ni kama ishara kwamba Shilole na Nuh kila mmoja amepata mrithi wa nafasi walizoziacha wazi baada ya kuachana.
Post a Comment