Mwanasheria
wa Serikali Mkoa wa Katavi pamoja na askari magereza wawili
wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani humo kwa tuhuza za kula njama na
kisha kumtorosha kwa siku 124 mtuhumiwa wa kesi ya kujaribu kumuua
mlemavu wa ngozi (Albino) baada ya kupokea rushwa ya jumla ya Sh3
milioni.
Tukio
la kutoroshwa kwa mtuhumiwa huyo linadaiwa kufanyika Oktoba 12 mwaka
jana, baada ya kupokea fedha kiasi hicho ambapo Mwanasheria wa serikali
mkoani Katavi, Falhati Seif Khatibu(45) alipokea kiasi cha Sh2 milioni
na askari Magareza A.287 S/SGT- John Masagula(50) pamoja na A. 5385 SGT
Deogratius Katani(50) wakigawana kiasi cha Sh milioni moja.
Kamanda
wa polisi Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari alisema kuwa kukamatwa
kwa watuhumiwa hao kulifanikiwa kutokana na taarifa za siri kutoka kwa
raia wema ambao walidai kuwa kuna mtuhumiwa aliyekuwa anashikiliwa
ametoroka kutoka katika gereza la mahabusu la Mpanda lililopo mkoani
humo.
Alisema
baada ya taarifa hizo ndipo uchunguzi ulipofanyika Januari 19 mwaka
huu, na kubaini kuwa mtuhumiwa Alex Manyanza(27) ambaye alikuwa
anashikiliwa kwa tuhuza za kujaribu kumuua kwa kumkata kiganja cha mkono
mlemavu wa ngozi Limi Luchoma(30), mwanzoni mwa mwaka na kufunguliwa
shitaka namba MTO/IR/76/2015 alikuwa ametoroka mahabusu.
Baada
ya upelelezi ilibainika kuwa ndugu wa mtuhumiwa huyo ndio waliotekeleza
mpango huo na kisha kumtorosha mtuhumiwa na kwenda kumficha katika
kijiji cha Kipande kilichopo mkoani Rukwa, na ndipo walipompa fedha hizo
mwanasheria mkuu wa serikali ili amuondelee shitaka linalomkabili
mtuhumiwa huyo baada ya kufanikiwa kutoroka gerezani.
Alisema
mtuhumiwa ni mzoefu kwa vitendo vya kutoroka gerezani kwani kabla ya
kufanya tukio hilo alikuwa ametoroka katika gereza la Kalila Nkulunkulu
lililopo mkoani humo, ambapo alikuwa anatumikia kifungo cha miaka mitano
jela baada ya mahakama kumtia hatiani kwa kosa la wizi wa mifugo.
Post a Comment