Mkufunzi wa Manchester United Louis
Van Gaal amesema kuwa atakata tamaa iwapo Manchester United ilifanya
mazungumzo na Jose Mourinho.
United haikutoa tamko lolote baada ya
ripoti hizo za juma lililopita kwamba maafisa wa kilabu hiyo walifanya
mazungumzo na wawakilishi wa aliyekuwa mkufunzi wa Chelsea Jose
Mourinho.
Alipoulizwa iwapo anafikiri kulikuwa na mazungumzo,Van
Gaal alisema: katika soka hilo linawezekana,lakini sidhani kama kulikuwa
na mazungumzo.
Amesema kuwa alikuwa na uhusiano mzuri na mkurugenzi mkuu wa United Ed Woodward na mmiliki Glazers na kwamba wangemwambia.
Manchester
United kwa sasa hawako katika michuano ya kilabu bingwa Ulaya,na wako
nafasi ya tano katika jedwali la ligi ikiwa pointi sita nyuma ya
manchester City ambao wako katika nafasi ya nne.
Van gaala amebaye alichukua ukufunzi wa kilabu hiyo 2014 na kuiongoza
United katika nafasi ya nne mwaka uliopita alikubaliana na pendeko
kwamba nafasi nyengine ya nne itaonekana kama mafanikio.
United itachuana na Sunderland katika uwanja wa Stadium of light siku ya jumamosi.
Post a Comment