Ligi kuu Tanzania kuendelea tena
Mshikemshike wa ligi kuu Tanzania bara utaendelea tena wikiendi hii ambapo jumamosi kutapigwa jumla ya michezo mitano.
Stand United watakua wenyeji wa Wekundu wa msimbazi Simba Sport klabu, huku Mgambo Jkt wakipimana ubavu na African Sport.
Mbeya City wao watakua katika dimba lao la sokoine mjini Mbeya, kuwaalika wanakishamapanda timu ya Toto Afrikans toka Mkoani Mwanza.
Majimaji watakuwa wageni wa Ndanda Fc mchezo utakaopigwa kwenye dimba la Nangwanda sijaona huko mkoani mtwara, Jkt Ruvu watakipiga na Kagera Sugar.
Ligi hiyo itaendelea tena siku ya jumapili kwa michezo miwili kuchezwa Mwadui Fc watapima ubavu na Tanzania Prisons, huku Coastal Union wakiwaalika Azam Fc.
Post a Comment