Muhimu: Taarifa ya Baraza la mitihani kuhusu matokeo ya kidato cha Nne 2015.
Baraza la Mitihani la Tanzania limekuwa likipigiwa simu na watu mbalimbali wakiomba ufafanuzi kuhusu taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi imetangaza kuwa matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) 2015 yamezuiwa kwa muda hadi tarehe 08/03/2016.

Baraza la Mitihani la Tanzania linapenda kuwajulisha watahiniwa na umma kwa ujumla kuwa taarifa hizo ni za UONGO na zinalenga kupotosha umma na kuleta taharuki.

Hivyo, Baraza linaomba umma kuzipuuza taarifa hizo kwa kuwa Wizara haijasitisha utoaji wa matokeo hayo. Matokeo yatatangazwa mara tu mchakato utakapokamilika.
Imetolewa na,
AFISA HABARI NA UHUSIANO

Post a Comment