Wasanii nchini wamekumushwa kuwa njia pekee ambayo itawawezesha
kuwa na mafanikio katika fani zao ni kufanya kazi kwa heshima bila
kubaguana huku wakitambua kuwa hawawezi kuwa ‘matawi ya juu’ siku zote.
Hayo yamesemwa na mwanamitindo na muimbaji,Jokate Mwegelo,ambaye
amewataka wasanii kutumia umaarufu wao vizuri ili wapewe ushirikiano na
kila mtu katika kazi zao.
”Nimesema hivyo kwa sababu baadhi ya wasanii wanavimba kichwa baada
ya kupata umaarufu hali ambayo mwisho wao huwa ni mbaya kwenye kazi
zao,”
”Msanii akiwa maarufu kila mtu akawa anaimba nyimbo zake ni rahisi
kuvimba kichwa na kujiona yeye ndio yeye,anasahau kabla ya yeye kulikuwa
kuna watu ambao walikuwa juu yake,”alisema Jokate.
Jokate alisema kuwa njia pekee ambayo itawasaidia wasanii na hasa wa
muziki wa kizazi kipya ni kutambua umuhimu wao kwenye fani hiyo pamoja
na nafasi ya wasanii wenzao na kuacha kujiona ni bora kuliko wengine.
Post a Comment