dully-12


  Dully Sykes amedai kuwa awali alipanga kumshirikisha Diamond kwenye wimbo wake Inde aliofanya na msanii wa WCB, Harmonize.

Akiongea na kipindi cha 180 Power cha Sibuka FM, Dully alisema baada ya kuona Diamond yupo busy, kura yake ilimwangukia Harmonize.

“Huu wimbo kwanza nilipenda kufanya na Diamond,” alisema muimbaji huyo mkongwe.
“Lakini nikaona Diamond yuko busy sana nisimsumbue, nikaangalia after Diamond nani anastahili, nikaona Harmonize anafaa kati ya vijana niliowafikiria.”

Post a Comment