Nahodha wa timu ya taifa ya Argentina anayeichezea klabu ya FC Barcelona ya Hispania Lionel Messi, August 12 2016 ametangaza kubadili maamuzi kuhusu soka la kimataifa, baada ya awali kutangaza kustaafu kuichezea Argentina.
Messi alitangaza kustaafu kuichezea timu ya taifa ya Argentina baada ya kumalizika kwa mchezo wa fainali ya Copa America 2016 dhidi ya Chile na kupoteza mchezo huo, kutokana na Messi kupoteza fainali yake ya tatu mfululizo akiwa na Argentina aliamua kutangaza kustaafu kuichezea timu ya taifa.
August 12 2016 chama cha soka cha Argentina AFA kimetangaza Lionel Messi kubadili maamuzi yake na kuwa ataendelea kuichezea timu ya taifa ya Argentina kama kawaida, June 27 2016 Argentina alicheza mchezo wa fainali ya Copa America dhidi ya Chile na kufungwa kwa mikwaju ya penati 4-2.
Post a Comment