Mke
kutumia simu ya mumewe kwa baadhi ya wanandoa inaweza kuwa ni ishu ya
kawaida sana lakini kwa Mwanamke mmoja kutoka Umoja wa Nchi za Kiarabu
(UAE) amelazimika kulipa faini baada ya kukutwa akipekua simu ya mume
wake bila ruhusa. Taarifa zinasema kuwa mwanamke huyo alikua akihisi
mumewe kuwa katika mahusiano na mwanamke mwingine.
Mume wa
mwanamke huyo alimshtaki kwa kukiuka sheria ya usiri mitandaoni ” na
kwamba mkewe alitumia simu yake bila ruhusa na ni kosa. Mwanamke huyo
alitakwa kulipa faini ya $41,000 ambazo ni sawa na Milioni 68 za
kibongo.
Baada ya
kukiri kuwa ni kweli alifanya hivyo kwa kwa kuwa amekua akimuhisi mumewe
kuwa na mpenzi mwingine pamoja na faini hiyo mwanamke huyo ameripotiwa
kutolewa nje ya nchi kwa muda.
Post a Comment