Hatimaye
mtangazaji wa Clouds Fm, Gardner G. Habash amemjibu aliyekuwa mkewe,
Lady Jay Dee, aliyemtaka aombe radhi ndani ya siku saba kwa kauli
aliyoitoa iliyodaiwa kuwa imelenga kumdhalilisha. Katika majibu yake
amekana madai hayo.
Siku
chache zilizopita, Gardner alionekana katika kipande cha Video
akisherehesha tukio la kumsaka mrimbwende wa chuo cha Tanzania Institute
of Accountancy (TIA) jijini Dar es Salaam, ambapo alisema kuwa “yule binti sina tatizo naye, nimeshamkojoza kwa miaka kama 15 hivi…”, kisha wimbo wa ‘Ndindindi’ wa Jay Dee ukachezwa na DJ.
Kama
ilivyokuwa kwa Lady Jay Dee aliyetoa siku saba za kuombwa radhi kupitia
kwa mwanasheria wake Amani Tenga, Gardner amejibu kupitia mwanasheria
wake Stephen Axwesso.
Katika
barua yake kwa mwanasheria wa Lady Jay Dee, mwanasheria huyo wa Gardner
amekiri kuwa ni kweli mteja wake alizungumza maneno hayo alipokuwa
katika shughuli iliyotajwa, lakini alidai kuwa hakuna sehemu aliyomtaja
mkewe huyo wa zamani.
Alisema
kuwa madai ya upande wa Lady Jay Dee hayana mashiko na alimshauri
mwanasheria huyo kupitia upya sheria inayozungumzia wanandoa
waliotalakiana ili aweze kumshauri vizuri mteja wake kuhusu suala hilo.
Nakala ya barua hiyo pia imetumwa Clouds Media Group na kwa Rais wa Wanafunzi wa Chuo cha TIA.
Post a Comment