Bondia mwenye jina kubwa katika ulimwengu wa ngumi Manny Pacquiao May 19 2016 ameingia kwenye headlines baada ya kufanikiwa kushinda nafasi ya Seneta katika bunge nyumbani kwao Filipino, Pacquiao amefanikiwa kushinda nafasi hiyo kwa kura milioni 16.
Pacquiao anakuwa ni miongoni mwa watu 12 waliofanikiwa kushinda nafasi ya Seneta katika bunge la Filipino,
ushindi wa bondia huyo maarufu unatoa tafsiri huenda siku akapata
nafasi ya kugombea nafasi za juu za uongozi wa nchi hiyo hususani Rais.
Kama utakuwa unakumbuka vizuri Manny Pacquiao mwenye umri wa miaka 37 amefanikiwa kushinda mataji kadhaa ya Ubingwa ngumi, Pacquiao ndio bondia aliyepigana na Mayweather na kupoteza kwa point katika pambano linalotajwa kutazamwa na mamilioni ya watu duniani kote.
Post a Comment