Waziri
Mkuu Mstaafu wa awamu ya Nne Mhe. Mizengo Pinda ametoa wito kwa
watumishi wa Umma kufanya kazi kwa bidii na kuzingatia sheria na
taratibu ili kuendana na kasi ya serikali ya awamu ya tano ya
kuwahudimia wananchi na kukabiliana na umasikini.
Akizungumza wakati akifunga mkutano wa kikao cha ushauri cha mkoa wa Katavi(RCC), Pinda
amezishauri halmashauri kufuata taratibu za manunuzi na matumizi ya
pesa kwa maslahi ya Umma ili kupiga hatua katika maendeleo ya mwananchi
mmoja mmoja.
Mhe.
Pinda amesema licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali zinazowakabili
watumishi wa umma katika utendaji wao ila amewataka watanzania kujenga
tabia ya kutokukubali kuwajibishwa kutokana na ukiukwaji wa utumishi wa
Umma.
Aidha
waziri Mkuu huyo Mstaafu amewataka viongozi na Wananchi wa Mkoa wa
Katavi kuumunga mkono na kumuombea rais Magufuli katika jitihada zake za
kupambana na ufisadi ili kuleta maendeleo ambayo yalihodhiwa na watu wachache.
Mhe. Pinda ameongeza kuwa kwa mwendo
wa Rais Magufuli anaamini kuwa ndani ya kipindi chake cha miaka kumi
kama akifanikiwa kumaliza vipindi vyote basi kutokana na kasi yake
Tanzania itakua imepiga hatua kubwa za kiuchumi na kuwa ni moja kati ya
nchi zenye uchumi wa kati.
Post a Comment