Wimbo wake mpya ‘Bado’ ndio unasumbua sasa hivi kwenye stations
mbali mbali za Radio na TV, taarifa nzuri inabidi uifahamu kwamba mkali
huyu amekwisha kamilisha album na itaachiwa mwezi wa tatu mwishoni.
Akizungumza kupitia kipindi cha Hatua tatu cha Times Fm, Harmonize
amesema yeye kila siku huwa anafikiria kuandika na kufanya ‘ngoma’ mpya.
“Nashukuru mungu huwa natumia muda mwingi kuandaa kazi mpya,
nmeshakamilisha nyimbo za kukidhi album, inshaalah mwezi wa tatu
mwishoni ‘menejimenti’ yangu itakaa ili kuweza kuiachia” amesema.
Katika ‘line’ nyingine Mkali huyo ameweka wazi changamoto
walizozipata wakati wa kufanya video ya Bado, ikiwa ni pamoja na
kuharibu Piki Piki iliyotumika hali iliyowapelekea kulipa zaidi ya Dolla
4000.
Post a Comment